Posts

Showing posts from February, 2018

Upendo- Pillars of Faith Lyrics

Image
VERSE 1 Mbona chuki kati ya waumini, wapi upendo upendo ule wa kwanza Kwa nini sasa tuwe na utengano, ikiwa tumeokolewa kwa neema Tutaketi japa moja na Mungu, aliye mtoa mwana wake wa pekee Wapenzi ninawasihi tupendane ikiwa tu watoto wa Mungu *2
CHORUS Upendo huvumilia haujivunii, haukosi kuwa na adabu Hautafuti mambo yake kamwe, tena hufurahii udhalimu Ikiwa tuna upendo tu wake Mungu, wapenzi tutafte upendo *2
VERSE 2 Eeh Mungu wewe ni nguvu yetu ilete baraka kwetu sisi wana wako Haki yako iwe ni nguvu yetu, uwe faraja yetu hata kwa machungu Upendo na amani tujazie, undugu uzidi uhasama na kisasi Mbona majirani tunapigana tufunze upendo tukakumbatiane *2
CHORUS *5 Upendo huvumilia haujivunii, haukosi kuwa na adabu Hautafuti mambo yake kamwe, tena hufurahii udhalimu
Ikiwa tuna upendo tu wake Mungu, wapenzi tutafte upendo *5