Upendo- Pillars of Faith Lyrics
VERSE 1
Mbona chuki kati ya
waumini, wapi upendo upendo ule wa kwanza
Kwa nini sasa tuwe na
utengano, ikiwa tumeokolewa kwa neema
Tutaketi japa moja na
Mungu, aliye mtoa mwana wake wa pekee
Wapenzi ninawasihi
tupendane ikiwa tu watoto wa Mungu *2
CHORUS
Upendo huvumilia haujivunii,
haukosi kuwa na adabu
Hautafuti mambo yake
kamwe, tena hufurahii udhalimu
Ikiwa tuna upendo tu wake
Mungu, wapenzi tutafte upendo *2
VERSE 2
Eeh Mungu wewe ni nguvu
yetu ilete baraka kwetu sisi wana wako
Haki yako iwe ni nguvu
yetu, uwe faraja yetu hata kwa machungu
Upendo na amani tujazie,
undugu uzidi uhasama na kisasi
Mbona majirani tunapigana
tufunze upendo tukakumbatiane *2
CHORUS *5
Upendo huvumilia haujivunii,
haukosi kuwa na adabu
Hautafuti mambo yake
kamwe, tena hufurahii udhalimu
Ikiwa tuna upendo tu wake
Mungu, wapenzi tutafte upendo *5
Comments